Fahamu jinsi Tuishi Tena Foundation ilivyoanzishwa na msingi wa kazi yetu.
Tuishi Tena Foundation (TTF) ni taasisi isiyo ya kiserikali inayofanya kazi Tanzania Bara kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya kwa wafungwa, waliowahi kufungwa, vijana walio katika mazingira hatarishi, watu waliotengwa kijamii na familia zilizoathirika kutokana na athari za kifungo.
Taasisi inaamini kwamba kila mwanadamu ana uwezo wa kubadilika, kurekebisha maisha yake na kuwa raia mwenye mchango chanya katika jamii. Kupitia elimu, ushauri nasaha, mwongozo wa kiroho, mafunzo ya ujuzi, uwezeshaji wa kiuchumi na ushirikiano wa kijamii, tunalenga kujenga maisha mapya na jamii salama.
“Uzoefu wa miaka 16 gerezani ulizaa maono ya kuanzisha taasisi inayotoa matumaini, mwongozo na fursa ya kuanza upya.”
Jamii ambayo wafungwa, waliowahi kufungwa, vijana walio katika mazingira hatarishi, watu waliotengwa kijamii na familia zilizoathirika na kifungo wanaishi maisha yaliyorejeshwa, yenye uwezo na ushirikishwaji kamili katika jamii.
Kurekebisha, kurejesha na kuwawezesha watu walioathiriwa na kifungo na kutengwa kijamii kupitia ushirikiano na taasisi za marekebisho, serikali, jamii, familia, sekta binafsi na wadau wa maendeleo.
Heshima kwa utu na haki za binadamu
Huruma, upendo na kukubali mabadiliko ya mtu
Uadilifu na uaminifu
Uwajibikaji na uwazi
Kutobagua kwa misingi ya hali, historia au imani
Ushirikiano na jamii na wadau
Weledi na ubora wa huduma
Kutoangalia makosa ya jana, bali uwezo wa kesho